Saturday, 17 March 2018

W WAPO Social Media

MJUE MUNGU UNAYEMWABUDU-2

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

UTANGULIZI

Napenda kuwashukuru maelfu ya wasomaji wangu katika ukurasa huu kwa kujitokeza kwa wingi kupokea kile ninachowasilisha kwenu. Pamoja na mwitikio wenu mkubwa pia ninatambua kuwepo kwa mawazo pinzani, lakini yaliyoghubikwa na udhaifu katika uelewa wa lugha, hata kwenye maneno ya kawaida tu ambayo mtu wa kawaida anajua maana yake.

Mathalan, kuna madai katika mada iliyopita yenye kupinga ya kwamba maandiko ya Mathayo 28:19 yanayozitaja Nafsi za Mungu za “Baba, Mwana na Roho Mtakatifu " ati hayana maana ya “majina ya nafsi” bali yana maana ya “vyeo”!

Wakati nafahamu vizuri sana kuwa wapinzani hawa wanawakilisha kambi gani za nadharia; kwanza napenda kutoa majibu ya kukanusha kuhusu madai yao kwa kutoa elimu ya lugha kwa wasomaji wangu ambao kwa kutokujua wanaweza kupotoshwa na upinzani potofu unaorushwa kwenye ukurasa wangu.

Katika mada hii naitumia kujibu haya madai yenye kupotosha watu wasiojua lugha za kibiblia na historia ya kambi za upinzani dhidi ya fundisho la utatu wa Mungu katika Biblia.

TAFSIRI YA MISAMIATI NA MANENO YANAYOPOTOSHWA

Nataka tujikumbushe ya kwamba tunapotaka kupata maana ya misamiati ya maneno tunarejea kwenye Kamusi ya lugha husika. Ikiwa ni Kiswahili tunarejea Kamusi ya Kiswahili Sanifu na kama ni Kiingereza tunarejea Kamusi za Kingereza zinazoamini. Kwa utaratibu huu naomba kutoa tafsiri ya misamiati ya maneno ya “jina” na “cheo” kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu maana ya msamiati wa neno “jina” ni “neno la kumtaja mtu au kitu.” Na kwa kimombo ni a word or set of words by which a person, animal, place, or thing is known, addressed, or referred to . Na maana ya msamiati wa neno “cheo” ni “daraja la mtu katika kazi, au hadhi” .“a name that describes someone's position or job”

Kwa ufafanuzi huu tumethibitisha kwamba Mathayo 28:19 imeandikwa kwa “jina la…” neno lenye maana ya “mtu” (person) na wala sio kwa “cheo cha…” ambalo maana yake “daraja katika kazi”. Mathayo aliyeandika kuhusu ubatizo alimnukuu Yesu alivyowaagiza kuhusu tamko linaloambata na kitendo cha kubatiza katika maji likihusisha “majina Nafsi tatu za Mungu ambazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

TAFSIRI YA BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU KUWA MAJINA YA NAFSI NA SI VYEO

Sasa naona ni muhimu pia kupitia maana ya msamiati wa maneno ya “baba” na “Baba’, maneno ya “mwana” na “Mwana” pamoja na “Roho Mtakatifu. Tuanze na tafsiri ya neno “baba” ambalo tafsiri yake ni “mzazi mwanamume, au abu”. Kwa kiingereza ni; “a man in relation to his natural child or children.”Hata hivyo, neno lililotumika katika MT 28:19 ni “Baba” ambalo kwa kingereza ni “the Father” na kwa lugha asilia ya kiyunani ni “PATROS” ambalo maana yake halisi ni jina la “Mungu Baba”.

Tukija kwenye msamiati wa neno la kawaida kuhusu “mwana” Kamusi inalitafsiri kuwa ni “mtoto wa kiume” a boy or man in relation to either or both of his parents. Lakini neno lililotumika katika MT 28:19 ni “Mwana” kwa kingereza ni “the Son” ambalo maana yake ni Mwana pekee wa Mungu au Mungu Mwana (YH.1:18).

Kwa upande wa tafsiri ya msamiati wa neno “Roho Mtakatifu” ambalo kwa kiyunani ni HAGIOU PNEUMATOS lina maana ya “jina kati ya Nafsi tatu za Mungu mmoja ikitanguliwa na Nafsi za Baba na Mwana. Kwa kiingereza “The Holy Spirit” is one of the three persons in the one God, along with the Father and the Son (Jesus is the Son)”

KAMBI YA NADHARIA YA UNITARIANISM

Kwanini kumekuwepo na watu wenye kupinga fundisho la Nafsi tatu za Mungu mmoja katika Biblia? Kwa kuwapanua wasomaji wangu ambao hawajasoma historia ya migawanyiko ya tafsiri za maandiko, naomba nitumie fursa historia fupi ya chimbuko la utata huu kama ifuatavyo:

Fundisho la Nafsi tatu za Mungu Mmoja katika Biblia, limekuwa limezalisha kambi mbali mbali zenye nadharia pinzani na moja wapo maarufu inajulikana kama “Unitarianism” Hii ni kambi yenye kujumuisha theolojia na madhehebu ya kifamilia ilianzia Poland, kisha Transylvania, Uingereza na Wales kisha ikaingia Marekani.

Chimbuko la kambi ya nadharia ya Unitarianism linatokana na utata wa migongano ya kiimani iliyoibuka tangu tarehe 22/1/1556 nchini Poland, ambapo Piotr of Goniądz (Peter Gonesius), aliyekuwa mwanafunzi wa kipoland, alipoasi na kusema kinyume na fundisho la Utatu wa Mungu. Tamko la kuasi alilitoa kwenye mkutano wa Sinodi ya makanisa ya Reformed (Calvinist) nchi Poland katika kitongoji cha Secemin.

Baada ya mjadala mkali uliodumu kwa takribani miaka tisa, mnamo mwaka 1565, wapinzani wa nadharia ya utatu wa Mungu walitengwa kutoka kwenye Sinodi ya Kanisa la Reformed la Poland na wakaanza kujiendesha sinodi zao kama kanisa dogo. Hatimaye walipodhibitiwa kurejea kwenye nadharia ya utatu waliondoka na kuhamia Holland ambako ndiko walijitangaza kwa jina la Unitarian. Kati ya miaka 1665 na 1668 mjuukuu wa Socinus aliyeitwa Andrzej Wiszowaty Sr. alichapisha chapisho la Bibliotheca Fratrum Polonorum quos Unitarios vocant (Library of the Polish Brethren who are called Unitarians 4 vols. 1665–69).

Kanisa la Urinitarian huko Transylvania lilitambuliwa kwa mara ya kwanza na “the Edict of Torda” lililotolewa na Transylvania Diet chini ya PrinceJohn II Sigismund Zápolya (January 1568), kiongozi wake wa kwanza akiwa Ferenc Dávid askofu wa zamani wa kikalvinisti. Huyu ndiye alikwisha kuanza kuhubiri imani mpya inayopinga nadharia ya utatu. Jina hili "Unitarian" lilichapishwa kwenye majarida nchini Transylvania mnamo tarehe 25/10/1600 na kupata umaarufu zaidi mwaka 1638 kupitia chapishoo la recepta Unitaria Religio.

Vuguvugu hili lilipata umaarufu nchini Uingereza katika enzi za Enlightenment na kufanyika madhehebu rasmi mwaka 1774 chini ya waasisi wawili akina Theophilus Lindsey na Joseph Priestley, Hii ilianzia huko Essex Street Church jijini London

Mnamo mwaka 1782 huko Marekani imani ya Unitarian ilipokelewa katika kusanyiko la King’s Chapel, Boston na kuongozwa na James Freeman (1759-1835). Mnamo mwaka 1800, Joseph Stevens Buckminster alitawazwa kuwa mchungaji wa the Brattle Street Church huko Boston, ambaye alihamaisha kwa nguvu kupitia mahubiri na machapisho ya kisomi na Unitarian ikakua kwa haraka huko New England.

Siku hizi yako madhehebu yanayojitambulisha kuwa ni ya Kikristo, lakini yametafsiriwa kuwa ni imani potofu ikiwa ni pamoja na hii kambi ya Unitarianism. Huko mbele tuendako tunakuja na orodha ya majina ya makanisa yanayoagukia kwenye kambi hii na kuoonesha maeneo ambayo nadharia zao zimepotoka kimaandiko.

MAJIBU YA TAFSIRI POTOFU YA KIHISTORIA

Mojawapo ya madai ya kambi ya Unitarianism ni dhana inayodai kwamba Maandiko ya Mathayo 28:19 yaliingizwa kinyemela kwenye nyaraka za kale wakati wa Baraza la kwanza la Nikea mwaka 325 B.K.

Madai haya yanakanushwa na ushahidi wa kihistoria wa maandishi ya kale yakiwemo Didache yanayokadiriwa kuandikwa kati ya 50 B.K na 70 B.K ikiwa ni kabla ya miaka 300 BK. Nukuu kuhusu ubatizo katika Didache 7:1 inathibitisha ya kwamba “kuhusu ubatizo unatakiwa kubatiza kwa namna hii: baada ya kueleza haya yote, batiza katika jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu katika maji yanayotiririka. Kwa hiyo, Baraza la Nikea lisingeweza kuingiza kinyemela maandiko ambayo yalikuwa yakitumika kabla yake.

Ushahidi wa pili kihistoria tunaupata kutoka kwa Tertullain aliyezaliwa 145 B.K na kuingia Ukristo mwaka 185 B.K. na ambaye alikufa mwaka 229 B.K Yeye alikuwa mwanazuoni wa thelojia ya kiyunani na Kilatini na kwenye maandishi yake ananukuliwa akisema: “…baada ya kufufuka kwake aliwaamuru kubatiza katika jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu…”

Sehemu ya mada inayofuata ndipo tutandelea kupitia kuhusu suala la kuabudu na mazingira mapya ya kuabudia. Kama umesoma ujumbe huu nijulishe kwa ku-like post hii na kuwarushia wenzako pia. Ubarikiwe sana.

LATEST VIDEOS

Newsletter

Subscribe to Wapo Mission International weekly Newsletter.

Do you need JESUS as your personal savior?
If YES then Click HERE
Please rate our website

Need To Reach Us?

Email:

info@wapo.or.tz

Phone:

|+255 766 777 126 |
|+255 713 649 865 |
|+255 712 249 724 |
Do you need JESUS? Click here

Who's Online

We have 42 guests and no members online