Saturday, 17 March 2018

W WAPO Social Media

MJUE MUNGU UNAYEMWABUDU-1

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Kumjua Mungu tunayemwabudu lazima kuzingatie miongozo iliyotoka kwa Mungu mwenyewe. Kipindi cha Agano la Kale, torati ya Musa ndio ulikuwa mwongozo wa kumjua na kumwabudu Mungu. Hata hivyo, ni taifa la Israeli peke yake ndilo lilikuwa na hii fursa ya kumjua na kumwabudu Mungu wa kweli. Mataifa na makabila mengine ambayo si Wayahudi yalikuwa hayamjui wala kumwabudu Mungu wa kweli. Kipindi hiki cha Torati kilichukua muda wa miaka 1,500.

Ukomo wa mwongozo wa torati ulifanyika siku Yesu aliposulubishwa juu ya msalaba: “…ndipo aliposema, tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” (Ebr.10:9-10)

Kwa hiyo, katika nyakati zetu leo, ili tupate kumjua Mungu tunayemwabudu, Mungu amejitambulisha upya kupitia Agano Jipya ambalo mjumbe wake ni Yesu Kristo. Katika Agano Jipya Neno la Kristo ndio mwongozo kamili wa sisi kumjua Mungu Baba.

Kana kwamba hii haitoshi, kumjua Mungu Baba kupitia kwa Yesu Kristo, ni zaidi ya kujua Neno la Kristo kimaandiko tu. Ni lazima kumjua Yesu Kristo mwenyewe kibinafsi na kujenga uhusiano naye kwa imani na kuanza kupata mabadiliko ya kiroho, na kufanana na Yesu kwa tabia na mwenendo

KUMWABUDU MUNGU KUPITIA YESU KRISTO

Kumwabudu Mungu kupitia kwa Yesu Kristo kunatokana na usemi wake pale alipojitambulisha akisema: “…Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (YH.14:6)

Tunapomwabudu Mungu kupitia Yesu Kristo tunafanya hivyo kwa kufanya dua na sala zetu kupitia jina la Yesu Kristo kama ilivyoandikwa:

“Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote, amin, amin, nawaambia, mkimwomba Baba neno lo lote atawaba kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata furaha yenu iwe timilifu.” (YH.16:23-24)

Katika Agano la Kale, ibada za kiyahudi zilizingatia sheria za dhabihu na matoleo mbali mbali kupitia kwa makuhani wa kiyahudi waliosimamia ibada hizo kwa mujibu wa torati. Mambo yote yalifanyika kwa mwongozo wa torati.

Lakini sasa, katika Agano Jipya, mtindo wake wa kuabudu hatupitii kwa makuhani wa torati. Tunapitia kwa Kuhani Mkuu mpya ambaye ni Yesu Kristo na ndiyo maana tunapotaja jina lake kwenye sala na maombi, kwa kuwa yeye yuko mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu baba, basi sala zetu zinamfikia Mungu kupitia kwake!

MAZINGIRA MAPYA YA KUABUDIA

Mbali na mabadiliko ya ukuhani, mwongozo wa kuabudu nao umebadilika na pia hata mazingira ya kuabudia nayo yamebadilika. Katika Agano Jipya tunafuata mwongozo uliotolewa na Yesu Kristo mwenyewe:

“Yesu akamwambia, mama unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.” (YH.4:21) “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.” (YH.4:23)

Maandiko haya ni ushahidi wa mabadiliko ya mazingira ya kuabudia, na mitindo ya kuabudu. Yesu anathibitisha ukomo wa ibada za Agano la Kale na ujio wa ibada za Agano Jipya.

Wakati ambapo ibada za Agano la Kale zilifanyikia ndani ya hekalu lilikokuwepo jijini Yerusalemu; kwenye Agano Jipya, ibada halisi zinafanyikia “katika roho na kweli”! Haya ni mazingira mapya ya kiibada! Miili yetu ndiyo imefanyika hekalu la kuabudia ambamo Roho Mtakatifu husimamia ibada zetu. (1 Kor.6:19)

Sehemu inayofuata ya mada hii tutafanya uchambuzi kuhusu haya mazingira mapya ya kuabudia, ambayo ni miili yetu kama hekalu la kuabudia.

Kama ujumbe huu umekufikia nijulishe kwa ku-like post hii, na kisha warushie marafiki zako na wapate kufuatilia sehemu ijayo ya ujumbe huu. Ubarikiwe sana.

LATEST VIDEOS

Newsletter

Subscribe to Wapo Mission International weekly Newsletter.

Do you need JESUS as your personal savior?
If YES then Click HERE
Please rate our website

Need To Reach Us?

Email:

info@wapo.or.tz

Phone:

|+255 766 777 126 |
|+255 713 649 865 |
|+255 712 249 724 |
Do you need JESUS? Click here

Who's Online

We have 24 guests and no members online